Shirika la habari la AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran katika mkusanyiko mkubwa wa wananchi wanamapinduzi mjini Tehran katika maidani ya Azadi alisema: serikali kwa mara nyengine tena inafunga mkataba na wananchi wake kwa kuchunga misingi ya mapinduzi na mitazamo ya wananchi pia mtazamo wa msimamizi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran , heshima na utukufu ni wadhifa wetu kuyasimamia na kwaajili ya kuyafikia hayo tupo tayari kutoa hata ruho zetu.Naye aliendelea kusema kuwa mapinduzi yetu nikwaajili ya kupata utukufu, heshima na kuokoa uislamu katika ardhi yetu, kwani utawala wakifalme wazamani ulikuwa unalenga kufuta masuala ya imani na dini kwa wananchi, ama wanachi kwakutaka uhuru na kujisimamia walichagua jamhuri ya kiislamu kwalengo la kusimamisha dini.Rais Ruhaniy alisema: leo hii tupo na furaha kuwa baada ya miaka 35 siku hadi siku tunafikia malengo yetu tukiwa na heshima na utuku wa hali ya juu katika kufikia malengo makuu ya mapinduzi yetu.Rais huyo alisema leo ni siku ya furaha kwa watu wote wapenda haki duniani nakusema ni siku ya ushindi wa uislamu dhidi ya ukafiri na ubeberu duniani, kisha kusisitiza kuwa muda wote tutakapokuwa pamoja bila ya kuangalia vyama na vikundi vya kisiasa tutashinda kamatulivyoshinda hapo mwanzo na tunaendelea kuwashinda, ama iwapo tukaacha umoja wetu wa kitaifa na tukashikamana na vikundi tofauti tofauti maadui zetu wataweza kutusambaratisha, ama mpaka hivi sasa umoja wetu katika manufaa ya taifa ndio siri kubwa ya ushindi wetu na mafanikio yetu.Dokta Ruhaniy alisema nchi yetu sasa yaelekea katika utulivu nakusema katika kipindi cha miezi sita serikali yake imeweza kusitisha hali ya mfumuko wa bei za bidhaa kwakiasi Fulani ambapo utapungua mfumuko huo mpaka kufikia 25 mwishoni mwa mwaka huu.Ama kuhusu suala la nyukilia alisema: serikali ya Iran ilikuwa inataka kuuthibitishia ulimwengu kuwa wao sikama hawataki kufanya sulhu na Marekani bali hawana imani na ahadi za Marekani, nakusema haki ya kurutubisha yureni ni haki ya msingi ya taifa la Iran pia vitisho vyao havitaweza saidia chocho kunako maamuzi ya wananchi, na vitosho hivyo ni masuala ya kitoto yaliopitwa na wakati.
10 Februari 2014 - 20:30
Msimbo wa Habari: 505173
Katika sherehe ya kutimiza miaka 35 ya mapinduzi ya Iran Rais wa Iran amesema: ushindi wa Iran ni ushindi wa umoja na mshikamano wa taifa, na kudumu kwake ni kwakuwa baada ya mapinduzi muda wote tuliokuwa pamoja, mapinduzi yetu yalikuwa ni ushindi wadamu kwa upanga, risasi haikuishinda risasi bali upendo uliishinda risasi